Tuesday, December 18, 2012

ARSENAL YAIZABA READING 5-2 CARZOLA APIGA HAT-TRICK

Mshambuliaji mahiri wa Uhispania Santi Carzola ametupia kambani mabao matatu"Hat-trick" Arsenal ilipoizaba na kuikandamiza kabisa timu iliyopo mashakani katika ligi ya Reading 5-2 na kuipeleka mpaka nafasi ya 15.

Arsenal wakiwa na kumbukumbu ya kunyanyaswa na Bradford katika kombe la ligi wiki iliyopita walitandaza soka la kuvutia.

"It was important to stay strong and play football. Success comes with playing football," Arsenal manager Arsene Wenger aliiambia Sky Sports. "And it was a very convincing win tonight."

Mjerumani Lucas Podolski ndie aliefungua mlango katika dakika ya 14 likiwa ni goli lake la 5 katika ligi kabla ya Carzola kupiga mbili katika kipindi cha kwanza .

Arsenal sasa ina point 27 tayari imecheza michezo 17,point 2 nyuma ya mahasimu wenzao Tottenham Hotspur na 15 nyuma ya Manchester United. Reading inashikilia mkia ikiwa na pointi 9.

Walcott alipigilia msumari mwingine dakika 8 baadaee pale alipoichachafya ngome ya Reading na kumchambua mlinda mlango Adam Federici.

Dakika ya 32 Podolski alifanya kazi nzuri na kumchungulia Carzola akiingia eneo la hatari na bila ajizi alimpenyezea pasi murua nae bila kupepesa macho akakandamiza mpira wavuni, goli hili ni ushahidi tosha wa ubovu wa safu ya ulinzi ya Reading .

Goli la nne kazi nzuri ya Gibbs kumdodoshea mpira wa kichwa Podolski eneo la hatari nae akamuona Carzola amekaa uzuri na kumuachia pande na Carzola kutupia bao tamu sanaaa.

Dakika ya 14 wakitokea mapumziko Carzola anatupia bao la 3"Hat-trick" shukran za pekee zimuendee Wilshere anaempenzezea pande murua Podolski nae kama kawaida anmsusia ngoma Carzola nae bila kupepesa macho anatupia kambani goli la 5 na la mwisho.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ni katika kombe la ligi Arsenal ikiwa nyuma kwa mabao 4-0 wanarudi mchezoni na kupitia muda wa nyongeza wanaichabanga Reading 4-7.

Le Fondre alifanya kazi nzuri dakika ya 66 alipomhadaa kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny na kuandika bao la kwanza, zikiwa zimesaalia dakika 19 mpira uishe Kebe nae akatupia kambani bao la pili na mpaka mwisho Arsenal 5-2 Reading.
Podolskiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii


Walcoooooooooooooooooooooooooooooooooooootttt


Carzola na wenzake wakishangilia goli

S.Carzola akielekeza mashambulizi langoni mwa Reading



Goooooaaaal, Carzola akifunga goli kwa kichwa


Kocha wa Reading Brian McDemott akiwa haamini kilichotokea


Kocha wa Arsena Arsene Wenger akimpongeza Theo Walcott kwa kazi nzuri aliyoifanya

ARSENAL 5-2 READING

No comments:

Post a Comment