Tuesday, December 18, 2012

KATONGO MWANASOKA BORA BBC 2012 AWABWAGA DROGBA,YAYA TOURE NA DEMBA BA

Naodha huyo wa Zambia mwenye miaka 30 amemshinda Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yahya Toure na kuwa mshindi wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika katika historia ya mashindano hayo.
Orodha ya washindani hao ilitangazwa na wataalamu wa soka Afrika, ambao wamezingatia umahiri wa mchezaji, uwezo wa kiufundi na ushirikiano na wachezaji wengine.


Christopher Katongo akipokea tuzo ya BBC ya mwanasoka bora wa Afrika 2012


Katongo na tuzo ya BBC


Katongo akibusu kombe la mataifa ya Afrika

Na idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku asilimia 40 kati yao wakimchagua Katongo, ambaye anachezea timu ya China Henan Construction.
Katongo ameweka rekodi mpya ukizingatia kwamba wachezaji wote walioorodheshwa katika kinyang'anyiro hicho walikuwa na mwaka wa mafanikio, wanne kati yao walikuwa wameshinda medali mbalimbali, ni Katongo pekee ambaye mafanikio yake yamezingatiwa na mashabiki wa mpira Afrika.

Katongo, ambaye ni mwanajeshi nchini Zambia, alikuwa kivutio pale alipoiongoza Zambia, katika michuano ya kombe la Mataifa Bingwa barani Afrika mnamo mwezi Februari mwaka huu.

Alifunga magoli matatu katika fainali iliyoandaliwa nchini Equatorial Guinea na Gabon na baadaye kufunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa penalti na kuisadia Zambia kubeba kombe hilo.

Zambia iliishindi Ivory Coast kwa 8-7 katika fainali hiyo baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu baada ya muda wa kawaida na muda wa ziada mjini Libreville.

MATUMAINI YA ZAMBIA KUELEKEA BRAZIL
Kilikuwa ni kipindi kilichojawa na hisia kwa Zambia, ambayo miaka 19, iliyopita ilipata msiba mkubwa, pale ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa timu ya taifa ilipoanguka mita 500 tu kutoka Libreville, na kuuwa wachezaji wote 25 pamoja na rubani wa ndege hiyo.

Miezi saba baada ya kuoingoza Zambia kushinda kombe hilo, Katongo pia ameng'ara katika michuano ya kufuzu kwa fainali za mwaka ujao,wakati alifunga goli la pekee dhidi ya Uganda.

Bao hilo lilikuwa bao muhimu sana kwa Zambia kwa kuwa ilipoteza mechi iliyofuatia kwa kuchapwa bao moja kwa bila, lakini ikafuzu kwa fainali za mwaka 2013 zitakazofanyika Afrika ya Kusini baada ya kushinda kwa magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti.

WAJIPANGA KUFUZU KWA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA
Na zaidi ya hayo yote, Katongo amechangia kwa kiasi kikubwa harakati za kufufua matumaini ya Zambia kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014.

Chris  Katongo
Naodha wa Zambia Chris Katongo

Zambia ililazwa magoli 2-0 na Sudan mjini Khartoum mwezi Juni, matokeo ambayo hadi wakati huu hayajathibitishwa, huku uchunguzi ukiendelea kuhusu hatua ya Sudan ya kumchezesha mchezaji ambaye hakusajiliwa.

Wiki moja baada ya mechi hiyo Zambia ilikipiga na Ghana na Katongo kwa mara nyingine ndiye aliyetupia kambani bao la ushindi na hivyo kuimarisha matumaini yao ya kufuzu.

Ikiwa Christopher Katongo ataendelea kuwa katika kiwango alichonacho kwa sasa, huenda akaisaidia Zambia kupata matokeo mazuri wakati wa michuano ya kuwania kombe la dunia nchini itakayoandaliwa nchini Brazil miezi kumi na minane ijayo.

Katongo katikati akiruka sarakasi kushangilia moja ya magoli yake

Katongo akifanya mambo dimbani
Video Katongo akifanya vituuz graundini

No comments:

Post a Comment