Monday, January 28, 2013

CLUB YA USIKU YA KISS YATEKETEA KWA MOTO WATU 233 WAFARIKI DUNIA

Raia wa Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa kusini wa Santa Maria.

Maafisa wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .

Wengine zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.


Baadhi ya ndugu ya waliopoteza maisha wakilia kwa uchungu

Maswali sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano

Familia za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.

Mazishi ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti ya nchi humo.

Maafisa wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia kutotambuliwa.

Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati ya umri wa miaka16 na 20.

Zaidi ya watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa.

Watu wakitimua mbio wakati moto ukiendelea kuwaka ukumbini hapo






Vikosi vya zima moto vikijaribu kuzima moto katika club ya disco ya Santa Maria








































No comments:

Post a Comment