Monday, January 7, 2013

KOMBE LA FA SWANSEA YAIBANA MBAVU ARSENAL

Timu ya Swansea imeilazimisha sare klabu ya Arsenal ya magoli 2-2 ikiwa ni raundi ya tatu ya kombe la chama cha soka nchini England (FA Cup) Magoli ya Swansea yalifungwa na Michu dk ya 57 na kuifanya Swansea kuongoza na kuifanya furaha ya mashabiki wa Swansea kudumu kwa muda wa dakika 23 kabla ya Lucas Podolski kuisawazishia Arsenal katika dakika ya 80.
Arsenal baada ya kusawazisha goli waliendelea kulisakama lango la Swansea na katika dakika ya 82 Kieran Gibbs aliwanyanyua vitini mashabiki wa Arsenal kwa kutupia bao la pili kabla D Graham hajawakalisha kwenye viti kwa unyonge pale alipotupia bao la kusawazisha katika dakika ya 86.
Na mpaka mwisho Swansea 2-2 Arsenal ngoma ikawa ngumu baina ya wakali hao katika kombe la FA.

Podolski akitupia fataki kuandika bao la kuongoza.




Michu akitupia bao la kusawazisha


Gibbs akiachia nduki kuandika bao la pili la Arsenal


D Graham akishangilia baada ya kusawazisha goli la pili.


Michu akishangilia bao
Swansea 2-2 Arsenal

No comments:

Post a Comment