Monday, January 7, 2013

REAL MADRID YAIBANGUA REAL SOCIEDAD,BARCA YAIADHIBU ESPANYOL 4-0

Klabu ya Real Madrid imeweza kufanya vyema katika Ligi kuu ya soka nchini Hispania mara baada ya kuibangua timu ya Real Sociedad kwa magoli 4-3.Magoli ya Madrid yalifungwa na Karim Benzema dk 1,Khedira dk 34  na magoli mawili ya Cristiano Ronaldo dk 67 na 69 huku magoli ya Sociedad yakifungwa na Xabi Prieto dk 8,39 na 75 Xabi alipiga "Hat-trick".


C.Ronaldo akitupia kambani

C Ronaldo akishangilia goli


Benzema akichanja mbuga
REAL MADRID 4-3 REAL SOCIEDAD
 
 

Katika mpambano mwingine Barcelona imeiangushia kichapo Espanyol cha mabao 4-0. Mabao ya Barca yalitupiwa na Xavi dk 9 kabla ya Pedro kuongeza mawili dk 14 na 26 na dakika mbili baadae mchawi wa kutikisa nyavu Leonel Messi alitupia kambani goli la nne dk 28.Mpambano huo uliohudhuriwa na mashabiki wapatao 95000 ulimalizika kwa Barcelona 4-0 Espanyol.


Messi na Sergio wakishangilia goli


Iniesta akichanja mbuga

Barca 4-0 Espanyol

No comments:

Post a Comment