Monday, February 4, 2013

MAN CITY "YANASANA" NA LIVERPOOL

Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Manchester City jana walishindwa kuendeleza mbio za kuifukuzia Man U kileleni pale walipolazimishwa sare ya mabao 2-2 na Liverpool katika dimba lao la nyumbani la Ettihad katika mpambano uliohudhuriwa na mashabiki wapatao 47,301.

Alikuwa ni Edwin Dzeko alieanza kuzifumania nyavu za Liverpool katika dakika ya 22 kabla ya Daniel Sturridge kuwanyamazisha mashabiki wa Liverpool katika dakika ya 28 ya mchezo. Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-1.

Katika kipindi cha pili alikuwa ni Mchezaji mkongwe Steven Gerrard alietupia mpira kambani na kuandika bao la 2 kwa Liverpool katika dakika ya 72 na kuamsha nderemo na vifijo katika dimba la Ettihad huku wenyeji wakiwa wanaona haya, Ilikuwa ni dakika ya 77 pale Aguero alipowapatia hafueni wenyeji kwa kutupia kambani bao la kusawazisha.
Mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa Man C 2-2 Liverpool.

Sturridge akifumua shuti lililoelekea moja kwa moja kambani

Nimeuaaaaa...Sturridge akishangilia goli

Imoooooo...Steven Gerrard akiachia nduki kuandika bao la pili


Nimeuaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Aguero akishangilia goli baada ya kumzidi maarifa Mlinda mlango wa Liverpool Reina
 
Man C 2-2 Liverpool
 

No comments:

Post a Comment