Monday, February 4, 2013

NIGERIA YAIFUNGASHIA VIRAGO IVORY COAST,BURKINA FASO YAIONDOA TOGO

Timu za soka za Taifa za Nigeria na Burkina Faso zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika.
Nigeria"Super Eagles" wametinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitungua timu ngumu ya Ivory Coast"Simba wa Teranga" katika mchezo uliopigwa katika dimba la Royal Bafokeng na kuhudhuriwa na mashabiki wapatao 25,000. Magoli ya nigeria yalifungwa na Emenike dk 42 na la pili lilifungwa na Mba dk ya 77, Huku lile la kufutia machozi la Ivory Coast likitupiwa kambani na Tiote dk 49 ya mchezo.

Burkina Faso wametinga hatua ya nusu fainali kwa kuiondosha timu ngumu ya Togo iliyokuwa ikiongozwa na Adebayor kwa goli moja kwa ubuyu, Goli likitupiwa kambani na Pitroipa dk 104 ikiwa ni muda wa nyongeza baada ya timu hizo kutoshana nguvu katika dakika 90. Katika mtanange huo uliomalizika kwa Togo kuondolewa katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika mashabiki wapatao 27,000 katika dimba la Mbombela walishuhudia Togo wakifungasha virago na kurejea nyumbani.

Pisha weweeeeeeee

Hapa kazi tuuu


Mba muuaji wa goli pekee la Burkina Faso


Kweli tumetoka!!!!!!!!!!!???????????



Kocha wa Nigeria Steven Kesh akishangilia kutinga nusu fainali

Huendi kokote weweeeeeeeeee

Adebayor akimwaga "udambwidambwi"

Burkina Faso wakishangilia baada ya kutinga nusu fainali

Ivory Coast 1-2 Nigeria
Burkina Faso 1-0 Togo

No comments:

Post a Comment