Monday, January 27, 2014

MICHAEL ESSIEN AMFUATA BALLOTELI AC MILAN

Kiungo machachari wa Chelsea mghana Michael Essien amekamilisha taratibu za usajili wa kuhamia AC Milan, pamoja na vyombo vya habari vya Italia kuripoti kuwa Essien alishindwa katika vipimo vya afya.

Essien aliekipiga Chelsea tangu msimu wa 2005 amesajiliwa na AC Milan ambapo atakipiga mpaka june 2015. Essien alisikika akisema “Just signed my contract to join one of the best clubs in the world. I’m very happy and looking forward to winning with the team.”

 Kocha mwenye vituko vingi wa Chelsea Jose Mourinho amesema “We would have been happy had he stayed because he is fantastic player for the team.”

 Essien mwenye umri wa miaka 31 atatangazwa rasmi kuwa mchezaji wa AC Milan siku ya jumanne (Kesho).


No comments:

Post a Comment