Thursday, January 23, 2014

PAPA AFUNGUKA INTERNET NI ZAWADI KUTOKA KWA MUNGU

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa Internet ni zawadi kwa dunia nzima kutoka kwa Mungu lakini akaonya kuwa matamanio ya kutaka kuwasiliana zaidi kutumia Internet kunawatenga watu kutoka kwa familia na marafiki zao.

Amewataka waumini wa kikatoliki kujiunga na mfumo wa dijitali. "Internet... inatoa nafasi ya mafanikio mengi. Hiki ni kitu kizuri bila shaka ni zawadi kutoka kwa Mungu,'' alisema Papa.

 

 

Katika ujumbe wake kwa dunia nzima ambao hutolewa kila mwaka, Papa amesema kuwa mfumo wa dijitali, unapaswa kuwa mtandao wa watu wala sio nyaya tupu.

Papa mwenyewe ana akaunti kwenye Twitter ambayo ina wafuasi zaidi ya milioni kumi.

Amehimiza kuwa mawasiliano yanapaswa kuhusisha hisia na mawazo, watu kukutana na kujuliana hali.

Kadhalika amewataka waumini wa kikatoliki kutodhani kuwa ni mawazo yao na imani zao pekee ambazo ni muhimu wakati wakiwasiliana na watu wa dini nyinginezo.

No comments:

Post a Comment