Kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania bara, Kim Poulsen, amewaacha
katika kikosi chake baadhi ya wachezaji wa muda mrefu wa timu ya taifa. Poulsen, kutoka Denmark, amewachagua wachezaji wapya kuwa miongoni mwa
wachezaji 22 wa timu ya Taifa Stars.
Kocha wa Stars Kim Poulsen
Juhudi hizo ni miongoni mwa maandalizi ya kocha huyo kwa mashindano ya kufuzu
kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014.
Ameamua kuwatema baadhi ya wachezaji wenye uzoefu wa muda mrefu na kuwachagua
vijana wadogo zaidi. "Nimeamua kuwachagua vijana hawa wadogo kwa kuwa ninaamini wataweza kuifanya
kazi hiyo ya timu ya taifa", alielezea. Kikosi cha Tanzania kina wachezaji; MaKipa: Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam), Deogratius Munishi (Mtibwa
Sugar) Walinzi: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah
(Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam),
Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba) Viungo wa kati: Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum 'Sure Boy' Abubakar (Azam),
Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward
Christopher (Simba), Mrisho Ngasa (Azam) Frank Domayo (JKT Ruvu) Washambuliaji:Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo),
Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Moro United), Haruna Moshi (Simba), John
Bocco (Azam) Poulsen aliwahi kuifunza timu ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17
na vile vile miaka 20, kabla ya kurithi kazi ya raia mwenzake wa Sweden, na
ambaye majina yanafanana, Jan Poulsen. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 ameamua kutowaalika wachezaji wa zamani
kama nahodha Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub, Henry Joseph, Nizal Khalfan na
Abdi Kassim. Kinyume na hayo, ameamua kumchukua tena mshambulizi mwenye umri mdogo Mbwana
Samata, ambaye huichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na
ambaye alikuwa ametupwa nje na kocha wa awali Jan Poulsen. Wachezaji wengine walioalikwa kujiunga na timu ya taifa kwa mara ya kwanza
miongoni mwa vijana waliopo katika timu ya chini ya umri wa miaka 20 ni pamoja
na Ramadhani Singano, Edward Christopher na Frank Domayo. "Kuna matumaini siku zijazo kupitia timu hii, na ninaamini mchezo wao
utastawi na kustawi", alielezea Poulsen. Kikosi kitaanza mazoezi yake kikiwa kambini kuanzia Jumatano, kwa nia ya
kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi, tarehe 26 mwezi huu wa Mei.
Wachezaji wa Man City wakishangilia ubingwa wa Uingereza
Manchester City ikifunga mabao mawili zikiwa zimesalia dakika mbili za nyongeza
mpira kumalizika, wamefanikiwa kuunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Kandanda ya
England kwa kuwalaza QPR waliocheza wakiwa 10 kwa mabao 3-2 katika mchezo
uliomalioza msimu kwa mtindo wa kusisimua.
Pablo Zabaleta alikuwa wa kwanza kuipatia bao la kuongoza Manchester City
kabla Joleon Lescott kufanya makosa na kumpatia nafasi Djibril Cisse
kuisawazishia QPR.
Kocha Mancini akishangilia pamoja na benchi la ufundi
Joey Barton alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kukwaruzana na Carlos
Tevez lakini alikuwa Jamie Mackie aliyeipatia bao la pili QPR kipindi cha
pili.
Huku Manchester United ikiwa imeshailaza Sunderland, Manchester City
walionekana kama wangepoteza nafasi ya kuunyakua ubingwa lakini Edin Dzeko
akafanikiwa kufunga bao la kusawazisha kwa kichwa na dakika moja baadae Sergio
Aguero akapachika bao la ushindi lililoimaliza kabisa QPR.
Kipa wa Man City Joe Hart akishangilia baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa Tevez akirushiana maneno na Joe Burton Kocha wa QPR Mark Hughes akiwa haamini kilichotokea
Hili ni taji la kwanza la Manchester City tangu waliposhinda kombe la Ubingwa
wa Ligi daraja la kwanza wakati huo mwaka 1968.
Manchester United imepoteza taji lake la Ligi Kuu ya England, licha ya
kuilaza Sunderland baada ya mahasimu wao wakubwa Manchester City kuilaza Queens
Park Rangers.
MAN C Vs QPR
Bao la kichwa lililowekwa kimiani na Wayne Rooney lilioneka kama lingempatia
Sir Alex Ferguson ubingwa wa Ligi Kuu ya Kandanda kwa mara ya 13 kwa kipindi
chake cha umeneja kwa miaka 20.
Manchester United walikuwa wanadhani wameshinda ubingwa baada ya Manchester
City kuwa nyuma kwa mabao 2-1 na zikiwa zinaelekea dakika za nyongeza kumalizika
huku mashabiki wao wakianza sherehe za ubingwa.
Man C vs QPR & Man U vs Sunderland Highlights
Lakini taarifa zilizofika kwa mashabiki wa Manchester United kwamba
Manchester City wamepachika mabao mawili ya haraka haraka dakika za mwisho
ziliwanyamazisha mashabiki hao na wachezaji wao wakaonekana hawaamini
wanachokisikia.
Arsenal imefanikiwa kupata nafasi ya tatu na watacheza Ligi ya Ubingwa wa
Ulaya msimu ujao moja kwa moja baada ya kuilaza West Brom mabao 3-2, hasa
kutokana na makosa ya mlinda mlango wa West Brom Marton Fulop.
Ushindi huo wa 3-2 ina maana kikosi cha Arsene Wenger kimemaliza msimu
wakishika nafasi ya tatu.
Koscielny akishangilia goli la pili na wenzake wa Arsenal
Fulop alifanya makosa yaliyoipatia Arsenal bao la kuongoza dakika nne tu
tangu mchezo ulipoanza kupitia kwa Yossi Benayoun lakini muda mfupi tu West Brom
wakafanikiwa kusawazisha.
Lakini walikuwa Andre Santos na Laurent Koscielny waliopiatia Arsenal mabao
ya ushindi kwa Arsenal.
Tottenham baada ya kuilaza Fulham mabao 2-0 imefanikiwa kumaliza ligi wakiwa
nafasi ya nne lakini watajipatia nafasi ya kucheza Ligi ya Ubingwa wa Ulaya
iwapo tu Chelsea itapoteza mchezo wa fainali ya Ubingwa wa Ulaya.
ARSENAL VS WBA
Emmanuel Adebayor alikuwa wa kwanza kuipatia Tottenham bao la kwanza ambapo
Fulham nao walikosa nafasi nzuri ya kufunga kwa mkwaju wa Moussa Dembele kugonga
mwamba.
Jermain Defoe aliithibitishia Tottenham ushindi baada ya kupachika bao la
pili kutokana na mkwaju wa awali alioufumua Aaron Lennon kuwagonga wachezaji wa
Fulham.
Ndoto za kucheza Ubingwa wa Ulaya kwa Newcastle ziliyeyuka baada ya Everton
kumaliza msimu kwa mtindo wa aina yake katika uwanja wa Goodison Park. Everton
walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1.
Steven Pienaar aliufungua mlango wa Newcastle kwa mkwaju wa yadi 20 ambao
ulimgonga mlinzi wa Newcastle Mike Williamson na kujaa wavuni.
Nikica Jelavic akaiongezea Everton bao la pili sekunde chache baada ya
jitahada zake za awali kupanguliwa na mlinda mlango Tim Krul kabla Johnny
Heitinga kuongeza bao la tatu.
Chelsea kwa urahisi iliilaza Blackburn mabao 2-1 baada ya kumiliki mpira kwa
muda mrefu katika uwanja wa Stamford Bridge.
Chelsea walipumzisha wachezaji wao wengi nyota wakiwa wanajiandaa kwa fainali
ya Ubingwa wa Ulaya wiki ijayo, lakini hata hivyo hawakuonesha kandanda ya
kuvutia sana.
John Terry aliufungua mlango wa Blackburn kwa bao la kichwa baada ya
kuunganisha mkwaju wa juu uliochongwa na Romelu Lukaku na baada ya dakika tatu
Raul Meireles akaifungia Chelsea bao la pili.
Chelsea walikosa nafasi nyingi za kufunga lakini Yakubu alionekana mwiba kwa
ngome yao baada ya kuipatia Blackburn bao moja katika shambulio la nadra
walilofanya.
Danny Graham akiwa amefunga bao lake la 100 tangu aanze kucheza kandanda
alifanikiwa kuipatia Swansea ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool.
Graham alifumua mkwaju akiwa karibu na lango zikiwa zimesalia dakika nne
kabla mpira kumalizika na kupata ushindi wa kumbukumbu.
Swansea walimiliki mchezo kwa muda mrefu kipindi cha kwanza na Gylfi
Sigurdsson mara mbili alikosa nafasi za kufunga.
Liverpool walibadilika kipindi cha pili na Andy Carroll mpira wa juu
alioupiga uliokolewa na mlinda mlango Michel Vorm.
Norwich walimaliza msimu vizuri sana baada ya kupata ushindi rahisi dhidi ya
Aston Villa hali iliyoongeza chagizo kwa meneja Alex McLeish.
Mshambuliaji wa Norwich Grant Holt alikuwa wa kwanza kuipatia timu yake bao
la kwanza kwa mkwaju wa adhabu ya moja kwa moja na kuandika bao lake la 17 msimu
huu.
Simeon Jackson alitumia makosa ya mlinzi wa Aston Villa Carlos Cuellar na
kupachika bao la pili akiwa karibu kabisa na lango.
Villa iliwalazimu wamshukuru sana mlinda mlango wao Shay Given, ambaye
alifanya kazi ya ziada kupunguza mabao.
Meneja wa Aston Villa McLeish alikuwa akizomewa na mashabiki wa timu yake
muda wote wa mchezo ambapo tangu ameichukua timu hiyo msimu huu mambo
hayakumuendea vizuri.
Bolton hatimaye wameshuka daraja na msimu ujao hawatacheza tena Ligi Kuu ya
Kandanda ya England baada ya kutoka sare na Stoke katika uwanja wa
Britannia.
Iwapo Bolton wangeshinda mechi hiyo - huku QPR wakiwa wamefungwa na
Manchester City - wangepona na shoka la kushuka daraja, lakini bao la mkwaju wa
penalti uliofungwa na Walters likaizamisha.
Mark Davies alikuwa wa kwanza kuipatia bao Bolton na baadae bao lililofungwa
na Kevin Davies likaonekana kabisa kufufa uhai kwa Bolton.
Lakini bao la penalti la Walters bada ya Peter Crouch, kufanyiwa rafu ndani
ya boksi likaididimiza Bolton na msimu ujao watacheza ligi ya Championship.
Wigan imefanikiwa kupata ushindi wa saba katika mechi tisa ilizocheza na
kuepuka kabisa panga la kuwateremsha daraja dhidi ya Wolverhampton Wanderers
ambao tayari wameshateremka daraja. Wingan wameshinda mabao 3-2.
Juma Nyosso wa pili kulia waliosimama akiwa na kikosi cha Simba
Beki mashuhuri Juma Nyosso wa Simba, amepata soko baada ya Klabu ya Platinum Stars ya Afrika Kusini kutangaza kuwa inataka kumnunua kwa ajili ya msimu ujao. Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa uongozi wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini (PSL), umeonyesha nia ya kumsajili Nyosso na ulifanya mazungumzo na Simba. “Kweli jamaa wa Platinum Stars walikuja na kufanya mazungumzo. Wameonyesha wanamhitaji Nyosso,” kilieleza chanzo cha uhakika na kuongeza “ Mazungumzo yalifikia katika hatua nzuri kabisa lakini kuna mambo kadhaa ya kuangalia ndipo hilo likamilishwe.” Mjumbe mwingine wa kamati ya usajili ya Simba aliliambia gazeti hili kuwa suala hilo lazima liidhinishwe na kamati ya usajili. “Kamati ya usajili itamaliza kila kitu lakini itafanya hivyo baada ya kukutana na kocha Milovan ambaye ataeleza anachokitaka, pia ni wachezaji gani anataka wabaki, waondoke au waongezwe. “Baada ya hapo tutaanza kufanya utaratibu, sasa inategemea huenda na Nyosso akaruhusiwa kuondoka,” alisema mjumbe huyo. Platinum Stars inayofundishwa na Owen Da Gama ipo katika nafasi ya 10 katika PSL na kikosi chake kina wachezaji wote raia wa Afrika Kusini isipokuwa watatu, kipa Etame Soppo (Cameroon), Henrico Boates (Namibia) na Mohammed Chikoto (Niger). Timu hiyo iliwahi kuripotiwa kumtaka Nyosso mwishoni mwa mwaka jana lakini baadaye viongozi wake walisita kuendelea na mazungumzo na Simba.
Sajuki akiwa kitandani na wasanii wenzake waliokwenda kumjulia hali
Masikini SAJUKI! Siku mbili kabla ya kwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India kwa matibabu, afya ya stadi wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ni ya kusikitisha ile mbaya. Kadiri siku zinavyoyeyuka, hali ya Sajuki inazidi kuwatoa watu machozi baada ya kuzidiwa na kushindwa kunyanyuka kitandani. Laiti kama utamuona na ukashindwa kububujikwa na machozi basi utakuwa huna utu. Wasanii wa Bongo movie wakiwa wamemzunguka Sajuki kitandani(Chini ya picha Wolper aliyetoa mil 15)
Tukio la kusikitisha lililowatoa machozi wasanii wenzake ni lile la Jumanne wiki hii nyumbani kwake Tabata Barakuda, Dar es Salaam ambapo msanii na prodyuza huyo wa filamu alishindwa kuamka kitandani kupokea dola elfu kumi (takribani Sh. milioni 15) alizozitoa mwigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper kwa ajili ya matibabu huku akisindikizwa na mastaa wengine wa Bongo Movie. Sajuki akiugulia maumivu huku akilalamika kujisikia vibaya, hivyo kuwaomba wasanii wenzake kwa heshima waingie chumbani kwake ili apokee fedha hizo.
Msanii wa Bongo movie akiwa ameshindwa kujizuia na kujikuta akimwaga chozi
Kitendo hicho ndicho kilichowafanya baadhi ya wasanii wenzake kushindwa kujizuia na kujikuta wakiangua vilio huku Sajuki akiwatuliza na kuwaomba wasilie wala wasihuzunike kwani kila kitu ni mapenzi ya Mungu. “Msihuzunike ndugu zangu, naamini kila kitu ni mapenzi ya Mungu na si vinginevyo, jipeni moyo,” alisema Sajuki kwa tabu akiwa amelala kitandani akiwa amezungukwa na mastaa hao. WOLPER Kwa upande wake Wolper aliyekuwa akimwaga machozi mithili ya bomba la mvua, alisema kuwa siyo kwamba ana fedha nyingi, ila ni namna alivyoguswa na mateso ya Sajuki. “Siyo kwamba sina shida bali ni moyo wa kusaidia kuokoa uhai wa mwenzetu. Tulizoea kuwa naye location (sehemu ya kurekodia filamu) na kwenye tasnia yetu, anaumwa na hajiwezi, niliumia sana,” alisema Wolper aliyekuwa akifutwa machozi na wenzake. WASTARA Naye mke wa Sajuki, Wastara Juma, huku akilia muda wote, alitoa shukurani zake za dhati kwa Wolper na kueleza jinsi alivyoguswa na kuona umuhimu wa kumsaidia mumewe Habari kwa hisani ya Global Publishers.
Mshambuliaji nyota wa zamani wa Manchester United, Quinton Fortune amefunguka kuwa yuko tayari kuifundisha timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 kama atapewa nafasi hiyo kwa sababu kiu yake ni kuona soka ya Kusini mwa jangwa la Sahara inakuwa na kufikia kiwango cha Afrika Magharibi na Kaskazini.
Quinton Fortune
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, Fortune alisema ingawa haifahamu rekodi ya timu ya Taifa ya Tanzania, lakini anaamini kama atapata nafasi ya kuifundisha timu ya vijana itakuwa ni faraja zaidi kwani atakuwa ametimiza kiu yake ya kufundisha soka na kuinua kiwango cha soka la Afrika ya Mashariki.
Fortune ambaye yuko nchini kwa lengo la kuzindua mashindano ya vijana ya Airtel Raising Stars, alisema anaamini wachezaji wa Ukanda huu wa Sahara wana matatizo yanayofanana na ndiyo sababu ya kushindwa kucheza soka katika ligi kubwa duniani kama England.
"Matatizo ya vijana wengi ni elimu ya soka, wana vipaji, lakini lazima upate elimu kwanza ili uweze kufanya vizuri katika soka,"alisema Fortune.
Fortune alisema tatizo lingine ni kushindwa kutafsiri mikataba mbalimbali ya soka, kushindwa kutambua umuhimu na malengo yao katika soka la kimataifa.
Alisema yeye alifanikiwa kucheza Ulaya kwa sababu aliondoka kwao akiwa na miaka 14 na kujiunga na klabu za huko ambazo zilimtunza kufikia hapo.
"Baada ya kumaliza kozi yangu ya ukocha pamoja na kumaliza kazi nilizopewa na klabu yangu ya Manchester United nitarudi Tanzania rasmi kwa ajili ya kufuatilia soka la Tanzania kwa undani zaidi pamoja na kutafuta vipaji na kufuatilia zoezi la Airtel Rasing Stars linavyoendelea pamoja na kuangalia maendeleo yao baada ya hapa,"alisema Fortune.
Mbali na Uzinduzi huo pia Fortune alitembelea Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongolamboto na kucheza soka na wanafunzi wa shule hiyo huku akikabidhi madawati 30 mipira 40 na jezi jozi tatu
Rais Barack Obama amesema kwamba watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana. Bwana Obama amesema daima amekuwa mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake
wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Marekani watendewe haki na jamii
kwa kutambua uhusiano huo, lakini amekuwa akipitia kile anachokiita mabadiliko
ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja. Ndoa ya jinsia moja ya kike
Kwa kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuunga mkono ndoa za
jinsia moja, suala ambalo limeleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Marekani.
Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa Wamarekani kuhusu kuunga mkono ndoa za
aina hii. Jamaa kaopoa kifaa anaona utaaaaaaaaaaaaamu
Rais Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa
muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita
katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja. Mapenzi ya jinsia moja yakiwa yamekolea ..wanaona utaaaaaaaaaaaaaaaaaaaamu
Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio
ya wote. Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha
Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja. Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni
yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia
moja. Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina
kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni
muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke. Waandamanaji wakidai ndoa za jinsia moko