Friday, August 19, 2011

MNARA UNAOTAJWA KUWA MREFU KULIKO YOTE DUNIANI WAANZA KUJENGWA

Ujenzi wa mnara unaotarajiwa kuwa mrefu kuliko yote ambayo imepata kutokea duniani umeanza, Unatarajiwa kupewa jina la KINGDOM TOWER. Mnara huo unajengwa nchini Saudi Arabia na unatarajiwa kuwa na urefu wa zaidi ya futi 3000 na unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola bilioni moja.
Mnara utakapokamilika muonekano uwapo mnarani utakuwa wa ajabu sana, ambapo ni zaidi ya 2/3 ya maili moja, utakuwa na maeneo ya biashara,maduka na sehemu za starehe.
Zifuatazo ni picha zitakazotokana na mnara huo pindi utakapokamilika.


 Tallest-tower
Manjonjo ya mnara huo sehemu ya juu na jinsi utakavyoonekan kwa mbele ukiwa Bahari ya Hindi.

Kingdom Tower
Taswira halisi ya mnara huo itakavyokuwa.


Tall Tower
Mandhari ya Kingdom Tower yatakavyokuwa sehemu ya chini.

JUKWAA LAANGUKA WAKATI WA TAMASHA LA MUZIKI NA KUUA

Nchini Ubelgiji jukwaa limeanguka na kuua watu kadhaa, Jukwaa hilo lilianguka katka tamasha la muziki linalojulikana kama Pukkelpop Music Festival jijini Hasselt, watu wanne wameripotiwa mapema kufariki dunia katika tukio hilo.

Belgium-Pukkelpop
Watu wakiwa wamepigwa na butwaa katika tukio hilo.

Msanii Cullen Omori amekaririwa mapema leo hii akisema "Ndio kwanza tulikuwa tumemaliza kuimba wimbo wetu wa kwanza katika nyimbo zetu hapa Pukkelpop, ndipo jukwaa na hema vikaanza kutingishika na tukafikiri labda ni kimbunga tu kinapita, ndipo nikaamrisha tuendelee na wimbo wa pili ndipo meneja wa msafara alisikika akipiga yowe kuwa tuteremke kutoka jukwaani, mara ghafla upande mmoja ukaanguka futi moja kwenda chini, tukafikiri kuwa ni jukwaa tu ndio limeanguka na sio hema ghafla vilio na kelele vilitosha kutueleza kilichotokea, lakini mpaka wanauja waokoaji na kututaarifu kuwa kuna watu waliopoteza maisha wapatao wanne na kadhaa wamejeruhiwa, huruma na mawazo yetu yakawa kwa wale waliowapoteza wapendwa wao katika janga hili."

Tazama jinsi ilivyokuwa

FAHAMU WATU MAARUFU WAMESEMA NINI WIKI HII

 photo | Jennifer Hudson
Jennifer Hudson "Najivunia kupungua uzito kuliko tuzo yangu ya Oscar"


 photo | Emma Stone, Jimmy Kimmel
Emma Stone amefunguka na kusema "It's a fake farm, but it doesn't feel fake, Jimmy. I was leaving dinners to harvest." Na kwa maneno hayo anasema ndio maana alijitoa Facebook.




 photo | Amber Heard
Amber Heard amefunguka na kusema "To say I came out implies that I was once in. Let me be straight about that – no pun intended [laughs] – I never came out from anywhere." Nyota huyo wa klabu ya Play Boy ameyasema hayo huku akitanabaisha kuwa huwa hafichi mahusiano yake lakini anapenda kuyafanya maisha yake binafsi kuwa ya siri.




 photo | Nicole Polizzi
Nae Nicole "snooki" Pollizi amefunguka na kushare na mashabiki wake mambo yake ya faragha kwa kusema "When I'm really excited about something, I poop."




 photo | Jimmy Kimmel, Kate Gosselin
Kate nae anafunguka hivi kuhusiana na suala la watoto "[Kate said] she will now devote more time to motivational speaking. Why not? She's already motivated millions of people to not have kids.





Caroline Gonzalez msichana mwenye umri wa nyundo 11 anafunguka na kusema "I like his music and I like him. And I thought, why not have a street in my hometown named after my favorite singer?"  Aliyasema hayo wakati akiupatia mtaa jina katika kitongoji cha Forney jijini Texas, alipochaguliwa kuwa meya wa siku moja.




 photo | Kim Kardashian, Tyra Banks
Tyra Banks nae anafunguka kuhusiana na harusi ya Kim Kardashian inayotarajiwa hivi karibuni "Nothing! A kiss and a congratulations."




BOB JUNIOR SIO SHOGA NI SANAA

Hivi karibuni katika vyombo vya habari vingi kumekuwa na habari ambayo imebamba vilivyo, nayo ni kumhusu mtayarishaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo flava,huyu si mwingine ni Rais wa Masharobaro Raheem Nanji a.k.a Bob Junior, ikisemekana kwamba kukatika kwake viuno katika kazi yake ya muziki kuna uhuziano na yeye kuwa shoga, Nimeshindwa kujizuia nikiwa shabiki wake namba moja na shabiki wa sanaa ya muziki huu wa bongo flava kusikia mtu akisingiziwa vitu ambavyo havipo kwasababu ya sanaa.

Raheem Nanji a.k.a Bob Junior

Huu ni ushamba kumtafsiri mtu tofauti na vile alivyo, kukata viuno ni kazi ya sanaa kwani wacheza show za muziki huwa wanafanya nini? hata hivyo wasanii wangapi duniani wanakata viuno? mbona hata Mr Nice enzi hizo alikuwa viuno kwa kwenda mbele,je ni shoga? H Baba nae hivyohivyo,je ni shoga? Fally Ipupa nae,je ni SHOGA? Acheni kufuatilia maisha ya mtu kama mnapenda muziki pendeni muziki kama hampendi kazi zake mpotezeeni acheni kumfuatafuata katika maisha binafsi. Hata kama ni shoga yanawahusu? kuweni basi na nyinyi mashoga kama mnamuonea wivu.

Elton John na wengine maarufu ni mashoga na wapo juu ile mbaya mbona hamsemi? acheni hizo kwanza nafikiri hamjui nini maana ya sanaa au nini maana ya msanii ndio maaana mnakurupuka na kumpakazia Bob Junior. Bob Junior kama unisoma hii mzee nakushauri makamuzi ya viuno kwa kwenda mbele asiependa kazi zako na akupotezee sio lazima awe fan wako, hiyo ni sanaa na lazima msanii aheshimiwe kulingana na hisia na mawazo yake, Bob Junior be more concerned with your character than reputation, because a character is what really you are and reputation is what people think you are...wapotezeeeeeee.
Labda kwa faida ya wasiojua nini maana ya msanii au sanaa,
Kwanza Sanaa ni dhima ya upangaji wa dhana kulingana na hisia na mawazo ya msanii,
Pili Msanii sasa ndio mtu anaepanga dhana kulingana na hisia na mawazo yake.

Sasa basi Bob Junior anahaki ya kufanya kazi vile hisia na mawazo yake yanavyomtuma ili kukamilisha kazi yake ya usanii na kazi hiyo isitafsiriwe kuwa ni ushoga kwani sanaa itabaki kuwa sanaa na ushoga utabaki kuwa ushoga na ndio maana nikasema Bob Junior ameona staili ya viuno ndio inaendana na hisia zake,basi tumheshimu kama kuna mengine hayahusu katika kazi zake, au mmepandikizwa na wasanii wanaomuonea wivu kwa kazi zake naweza kuwaelewa lakini sio kiivyo.

SONGI LA LEO

Linex na wimbo wa moyo wa subira

Thursday, August 18, 2011

TAZAMA VIDEO JINSI BARCA ILIVYOICHARAZA REAL MADRID


Iniesta akitia nyavuni bao la kwanza




Messi akitia kwenye kamba goli la pili


Benzema akiisawazishia Real goli la pili


Ronaldo akipachika bao la kwanza kwa Real Madrid


Marcello amchezea vibaya Fabregas



SIMBA YAILIZA YANGA 2 KWA BUYU

Sunzu akishangilia baada ya kutia kambani goli la pili

SIMBA, Simba ndio ulikuwa wimbo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada vijana hao wa mtaa wa Msimbazi kulipinza kisasi kwa ukifunga Yanga mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Simba waliofungwa kwenye Kombe la Kagame na Ngao ya Jamii mwaka jana vijana hao wa Mganda Moses Basena walizinduka na kupata mabao ya mapema kupitia kiungo Haruna Moshi 'Boban' dakika 15 na penalti ya Felix Sunzu dakika 38.

Simba iliyoanza kwa kasi mchezo huo ilifanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia kwa Moshi 'Boban' aliyemalizia vizuri krosi ya kutoka upande wa kushoto iliyopigwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Sunzu aliyekuwa na ushirikiano mkubwa na Emmanuel Okwi.

Mshambuliaji Sunzu alifungia Simba bao la pili kwa mkwaju wa penalti baada ya Nadir Haroub kumchezea vibaya Moshi 'Boban', kwenye eneo la hatari dakika 35. Sunzu alilazimika kuonyesha ueledi wake pale alipotakiwa kurudia penalti hiyo baada ya mwamuzi Israel Mjuni kusema Kado alitokea kabla ya kupigwa kwa penalti ya kwanza pamoja na kuwa alikuwa amefunga.

Kocha Moses Basena aliyeonekana kujifunza kwa makosa alitumia mfumo wa 4:2:3:1 na kutoa nafasi kubwa kwa Okwi, Haruna na Sunzu kutawala sehemu kubwa ya kiungo tofauti na ilivyokuwa kwenye fainali ya Kombe la Kagame.

Okwi alifanya atakalo mbele ya mabeki wa Yanga walionekana kuwa kama watu waliozidiwa na mazoezi na kukosa unyumbulifu mchezoni, huku safu ya ulinzi wa Simba chini ya mkongwe Victor Costa aliweza kuwapoteza mchezoni kabisa mshambuliaji Keneth Asamoah na Jerry Tegete.

Kiungo Haruna Niyonzima alijitahidi kuonyesha uwezo mkubwa wa kutawala mpira na kujaribu kutafuta goli kwenye mechi yake ya kwanza ya watani wa jadi, lakini alikosa msahada kutoka kwa wenzake.

Simba ilianza mashambulizi kwa kasi na dakika kwanza Okwi alikosa bao baada ya shuti lake kumgonga Haroub na kupaa juu ya goli.

Okwi alipoteza nafasi nyingine dakika 8 baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Yanga, lakini aliugonga mpira mbele zaidi na kipa Shaaban Kado akauwahi.

Beki wa Yanga, Chacha Marwa, nahodha Shadrack Nsajigwa alipewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Okwi. Naye Juma Nyoso wa Simba alipewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Asamoah.

Haruna Niyonzima alipiga shuti la umbali wa mita 25 baada ya kumchungulia Juma Kaseja kwa bahati mpira huo ulipaa juu ya goli.

Kipindi cha pili Yanga iliamka baada ya kuingia Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo lakini walishindwa kuipenya ngome ya Simba.

Yanga waliendeleza sera yao ya kugomea jezi za wadhamini wa ligi Vodacom zenye nembo nyekundu kwa kuvaaa jezi za mdhamini wao TBL tofauti na Simba wenyewe walivaa zile walizopewa na Vodacom

Vikosi Yanga;
Shaaban Kado, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Chacha Marwa, Juma Seif, Godfey Taita, Haruna Niyonzima, Keneth Asamoah/ Gumbo, Jerry Tegete, Kigi Makasi/ Kiiza.
Simba: Juma Kaseja, Said Nasoro, Amir Maftah, Juma Nyoso, Victor Costa, Partick Mafisango, Salum Machaku/ Kiemba, Jerry Santo, Felix Sunzu, Haruna Moshi/ Gervais Kago, Emmanuel Okwi/ Kapombe