Rafael Nadal (Kushoto) akiwa amebeba kombe la Ubingwa wa Italian Open baada ya kumshinda Djokovic(Kulia)
Rafael Nadal, mchezaji wa Uhispania, alifanikiwa kumshinda
mchezaji bora zaidi duniani wa kiume, Novak Djokovic katika mashindano ya Italia
Open, na kupata ubingwa wake wa sita katika mashindano hayo ya Italia. Nadal alipata ushindi wa 7-5 6-3 katika fainali hiyo ambayo ilichezwa
Jumatatu baada ya kuahirishwa siku ya Jumapili kutokana na mvua kunyesha mno
mjini Roma.
Ushindi huo umemweka Nadal katika nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji
bora zaidi katika mashindano ya wanaume duniani.
Pamoja na hali ya hewa kuwa si shwari lakini wapenzi wa mchezo wa Tennis waliendelea kufuatilia mtifuano huo kati ya Nadal an Djokovic
Kabla ya mashindano ya Jumatatu, Djokovic, raia wa Serbia, amekuwa akimshinda
Nadal mfululizo katika mashindano saba yaliyopita, kabla ya kuanza kuibuka tena
kama mshindi katika fainali ya Monte Carlo Masters mwezi uliopita. Sasa Nadal amemshinda katika fainali mbili za mwisho walizokutana. Nadal alisema: "Mawazo ya ushindi yalinijia wakati muwafaka, kwani kumshinda
Novak, unahitaji kuwa katika hali yako bora zaidi ya uchezaji, kwani yeye
hukusukuma hadi mjwisho katika pambano lote. "Nadhani kiakili nilikuwa katika hali thabiti kila wakati muhimu
nilipohitajika kuwa hivyo."
Wachezaji wa Chelsea wakiwa na mwali wa ligi ya mabingwa ulaya
Meneja wa mda wa Chelsea Roberto di Matteo alipoingia mkutano wa wandishi wa
habari kwa mazungumzo ya baada ya mechi saa saba na robo usiku wa manane,
akijivunia rekodi kubwa kwa meneja yeyote wa muda kuwahi kushinda, machungu ya
Chelsea daima kukosa Kombe la Ligi ya mabingwa tayari yalikua yamefutwa kwa dawa
nyepesi kutamka, Ushindi. Didier Drogba alipojipanga, bila pupa,wasiwasi wala hofu na kuupiga mpira ule
kumpita golikipa wa Bayern, Manuel Neuer, mwenye sifa ya kuzuia mikwaju ya
penati na kuthibitisha ushindi wa 4-3 kupitia matuta, miaka mingi ya kosa kosa
iliwatoka wachezaji wote,wafanyakazi na viongozi wa Chelsea.
Kocha wa Muda wa Chelsea Robert Di Matteo aliyeipa ubingwa wa barani ulaya Chelsea na kuweka rekodi ya kocha wa muda mwenye mafanikio zaidi
Hili lilifuatiwa na Drogba kuvua shati lake na kulipeperusha juu ya kichwa
chake kuonyesha furaha ya ushindi baada ya kukimbia kuzunguka uwanja mzima, huku
Fernando Torres na David Luiz wakipanda juu ya besera la goli kuonyesha furaha
yao. Wakati huo Mmiliki wa klabu hio Abramovich mwenyewe akiruka na kupiga
makofi huku akiimba ikidhihirisha sura isiyoonekana kwa kawaida kwa mtu msiri
asiyeonyesha hisia zake.
Drogba akishangilia baada ya kutupia kambani penati ya mwisho iliyoipa ubingwa Chelsea
Ikiwa mkwaju huo ulikua wa mwisho kwa mchezaji huyu kutoka Ivory Coast kama
mchezaji wa Chelsea, pamoja na bao lake la kusawazisha lile la Thomas Mueller,
basi Drogba ataondoka kwa kuweka rekodi yake binafsi. Drogba akimiliki mpira katika fainali hiyo
Drogba mwenyewe hakuweza kuelezea bayana juu ya majaliwa yake baada ya
kukabidhiwa zawadi ya mchezaji bora wa mechi hio ya fainali ya Ligi ya mabingwa
barani Ulaya. Punde mkataba wake unafikia mwisho na bado hakuna matumaini ya
kama ataongezewa mda. Hatma ya Meneja wa mda Di Matteo bado haijabainika na mwenyewe alishindwa
kusema ni nini alidokezewa na Abramovich walipokumbatiana kwenye ngazi kabla ya
sherehe za kukabidhiwa Kombe kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 107 ya
klabu hio. Haikua kazi rahisi kwa Chelsea uwanjani mpira ulipochezwa katika sehemu ya
uwanja ya Chelsea lakini hadi mwisho lakini waliepuka uwezekano mkubwa wa
kufungwa zaidi ya mabao manne ila kutimiza ndoto ya
Abramovich. Mara pekee kwa klabu hii kushamiri katika mashindano ya Ulaya, ulikua mwaka
1971 kabla ya hata Liverpool kushinda nje ya England, Chelsea ilipoichapa Real
Madrid na kujishindia Kombe la Mshindi la mwaka huo wa 1971. Drogba, aliongoza na kua kinara, na hivyo kuandika jina lake kwa vitendo
katika historia. Kipa Petr Cech amepitia kipindi kigumu wakati wa kampeni ya
Ligi ya mabingwa wa Ulaya lakini mjini Munich alionyesha ukomavu kwa kuzuia
mkwaju wa Arjen Robben katika kipindi cha ziada na wakati wa matuta alizuia
mkwaju wa Ivica Olic. Mwamko wa Chelsea ulianza pale alipotimuliwa Andre Villas
Boas kufuatia kipigo cha 3-1 na Napoli na mrithi wake Di
Matteo akageuka kua chachu ya ufanisi kwa kusababisha ushindi wa Kombe
la FA na mechi kadhaa za Ligi kuu ya Premiership. Matokeo ya Napoli yakageuka kuipendelea Chelsea na baada ya hapo kuichabanga
Benfica kujishindia fursa ya kukutana na Barcelona ambayo waliweza kuishinda kwa
hatua zote mbili,nyumbani na ugenini licha ya kusukumwa kwa dakika nyingi. Sifa kubwa anastahili Roberto Di Matteo aliyechimba ndani ya bongo za
wachezaji aliyewafahamu na kuamini kua wana uwezo wa kushiriki na kucheza soka
kwa kiwango cha juu na kushinda. Bila shaka wadadisi watakosoa mbinu zilizotumiwa dhidi ya Barcelona na huko
Munich lakini jibu la Di Matteo ni moja tu angalia rekodi ya mwaka 2012,
Mabingwa wa Ulaya ni Chelsea. Uwanja wa Allianz Arena ambapo kipute cha fainali ya ligi ya mabingwa kilipigwa na Chelsea kuibuka kidedea
Habari za kuthibitika kutoka ndani ya klabu ya Simba ya Dar es salaam ambao ni mabingwa wa soka Tanzania bara 2012-2013 zinasema jezi namba 30 iliyokuwa ikitumiwa na kiungo mkabaji marehemu Patrick Mutes Mafisango imepigwa "STOP" kutumika au kuvaliwa na mchezaji mwingine katika hali ya kumuenzi mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Rwanda.
Wachezaji wa Simba Uhuru Selemani na Yondani wakiwa katika majonzi hospitali ya muhimbili Uhuru Suleiman ameshindwa kujizuia akimwaga chozi katika hospitali ya Taifa Muhimbili
Patrick Mutesa Mafisango alifariki siku ya alhamisi alfajiri saa 10:25 akitokea Muziki kuelekea nyumbani kwake keko. Ajali hiyo ilitokea maeneo ya Tazara jijini Dar es salaam kwa kile kilichosemekana marehemu alikuwa katika jitihada za kuokoa maisha ya muendesha pikipiki ndipo alipojaribu kumkwepa kwa kuwa gari ilikuwa katika mwendo kasi iliacha njia na kuingia mtaroni na kupinduka na kusababisha kifo cha mchezaji huyo papo hapo na wenzake aliokuwa nao kwenye gari kujeruhiwa.
Mashabiki wa Simba na wapenzi wa Mafisango wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Hii ndiyo gari aliyopata nayo ajali Patrick Mutesa Mafisango
Kifo cha Mafisango kimeacha majonzi sio tu kwa Mashabiki na wachezaji wa Simba bali watanzania wote wapenda michezo na Wanyarwanda wote ambapo walikuwa wakimtegemea kwenda kujiunga na timu yao ya Taifa kupeperusha bendera ya Rwanda katika mashindano ya kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia.
Boniface Pawasa mchezaji wa zamani wa Simba ameshindwa kabisa kujizuia akitokwa na machozi mbele yake ni Uhuru Suleiman Wasanii wa kundi la Wanaume kushoto Chege na wenzake wakiwa msibani nyumbani kwa Mafisango Haruna Moshi "Boban" akiwa katika lindi la majonzi akimlilia Mafisango
Kitu cha kusikitisha na kuhuzunisha zaidi ni kwamba Patrick Mutesa Mafisango baada ya kuitwa kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Rwanda na kocha Micho, aliomba asogezewe siku kwani alikuwa ndio ametoka kushiriki mashindano ya kombe la shirikisho akiwa na timu yake ya Simba ya Dar es salaam. Alipokubaliwa Patrick Mutesa Mafisango alikuwa amepanga kuondoka Tanzania leo 18/5/2012 kwenda kujiunga na timu yake ya Taifa ya Amavubi lakini kwa masikitiko siku hiyohiyo aliyoipanga kwenda Rwanda kujiunga na Timu yake sasa anakwenda akiwa hana uhai tena...inasikitisha sana!! MUNGU AILAZE ROHO YA PATRICK MUTESA MAFISANGO MAHALA PEMA PEPONO..AMIN!
Kocha Mkuu wa Liverpool Kenny Dalglish ametimuliwa kuifundisha
klabu hiyo.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo inasema uamuzi huo umefikiwa baada ya
tathmini ya kina iliyofanywa.
"Baada ya kutathmini kwa makini klabu imefikia uamuzi na kuona mabadiliko ni
ya muhimu" Imesema taarifa hiyo
"Matokeo ya ligi kuu ya Premia yametusikitisha na katika kulinda maendeleo
yaliyopatikana ni lazima kufanya mabadiliko" Dalglish kuondoka kwake kwenye klabu ''kumefanywa kwa utu na heshima
kubwa''. Kocha Mkuu wa Wigan Roberto Martinez na Kocha wa zamani wa Liverpool Rafael
Benitez wanatajwa kuwa huenda wakachukua nafasi ya Dalglish. Dalglish anaelezwa kutokuwa na matokeo mazuri katika ligi kuu ya England. Kuondoka kwake kumekuja baada ya mazungumzo na wamiliki wa Klabu hiyo John
Henry na Tom Werner mjini Boston,Marekani siku ya Jumatatu. Zaidi ya Liverpool kufika fainali ya FA na kuchukua Kombe la Carling, timu
hiyo imemaliza ligi kuu ya England ikiwa nafasi ya nane huku ikipoteza michezo
mingi.
Kiungo wa zamani wa Simba s.c Marehemu Patrick Mafisango"Mutesa"
Kiungo mashuhuri wa Simba sports club Patrick Mafisango amefariki ghafla katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tazara amabapo ni kituo cha gari moshi linalounganisha nchi ya Tanzania na Zambia,wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
Chanzo cha ajali hiyo ni kitendo cha Marehemu Mafisango akiwa katika gari yake na mdogo wake alipojaribu kumkwepa muendesha pikipiki na katika harakati za kuokoa maisha ya muendesha pikipiki huyo hatimae gari la Mafisango liliacha njia na kuingia kwenye mtaro na kupinduka na kusababisha kifo cha mchezaji huyo wa Simba, katika ajali hiyo pia mdogo wake Mafisango alijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitalini.
"Kifo cha Patrick mafisango kimetusikitisha sana hasa kipindi hiki ambachio alikuwa katika kiwango cha juu sana ametuachia pengo wanasimba"Alisema mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alipohojiwa na kituo kimoja cha radiop nchini Tanzania. Patrick Mafisango enzi za uhai wake akilisakata kabumbu Mafisango akiwa amebebwa juujuu na wachezaji wenzake wakishangilia ushindi enzi za uhai wake Mafisango kulia enzi za uhai wake akishangilia goli pamoja na mwenzake Emmanuel Okwi Mafisango wa tatu kushoto waliosimama akiwa na kikosi cha Simba enzi za uhai wake Mafisango akiwa amejipumzisha baada ya mazoezi na timu yake ya Simba Mafisango katika swaga za kitaa enzi za uhai wake